Kituo cha Taarifa za Dharura Zinazotumika
Wakati wa janga au dharura, tembelea ukurasa huu ili kupata taarifa rasmi za karibuni zaidi kutoka kwa Jiji la Austin na Kaunti ya Travis kuhusu hatari inayoikabili jamii yetu na hatua za haraka unazopaswa kuchukua ili kukuhifadhi wewe na wapendwa wako salama. Zingatia kualamisha kiunganishi cha ukurasa huu ili uweze kukipata kwa haraka wakati wa janga. Unaweza pia kufuata Austin HSEM katika mitandao ya kijamii:
Twitter - @AustinHSEM
Facebook - @AustinHSEM
Jitayarishe Sasa kwa Ajili ya Dharura
Njia bora zaidi ya kujilinda mwenyewe wakati wa dharura kuu ni kuwa na mpango wa usalama, vifaa, na ufikiaji wa taarifa muhimu muda mrefu kabla haijatokea.
Tembelea ReadyCentralTexas.org ili kujiandikisha kupokea taarifa za dharura, na ujifunze unachoweza kufanya leo ili kujisaidia mwenyewe kuokoka na kupona kwa haraka zaidi kutokana na majanga katika siku zijazo.
Ofisi ya Msajili wa Msaada wa Dharura wa Jimbo la Texas
Jisajili kwa Ofisi ya Msajili wa Msaada wa Dharura wa Jimbo la Texas (STEAR). Jisajili kwa STEAR ikiwa wewe, mwanafamilia au rafiki ana hali ya kiafya, mahitaji ya kutembea, au mahitaji ya mawasiliano yanayohitaji msaada wa ziada wakati wa tukio la dharura.
Pakua Programu ya Ready Central Texas
Ofisi ya Jiji la Austin ya Usalama wa Nchi na Usimamizi wa Dharura na Ofisi ya Usimamizi wa Dharura ya Kaunti ya Travis zimeshirikiana kuanzisha programu ya simu ya matayarisho ya dharura.
Programu ya Ready Central Texas huandaa:
- Ripoti za habari na maonyo
- Habari za maandalizi
- Orodha za ukaguzi za mpango wa dharura ili kusaidia kuhakikisha kwamba una kile unachohitaji
Programu hio inapatikana kwenye vifaa vya Android na iOS na ni bure kupakua na kutumia.
Hali
Hali hatari zinaweza kuathiri watu, mali, na wanyama-vipenzi. Ikiwa bado hujafanya hivyo, chukua tahadhari sasa. Endelea kufahamu hali ya hewa, fuatilia habari za eneo lako.
Utabiri wa Huduma ya Kitaifa ya Hali ya Hewa.
Hatari Inayoweza Kuongezeka ya Moto wa Msituni
Huduma ya Kitaifa ya Hali ya Hewa imetoa Onyo la Bendera Nyekundu kwa eneo letu ikimaanisha kwamba kuna hatari ya moto wa msituni katika eneo la Austin na Kaunti ya Travis. Fuata maagizo rasmi ya dharura, kaa macho, na uwe tayari kuhama ikihitajika. Zifuatazo ni baadhi ya tahadhari ili kubaki salama wakati wa tukio hili:
Fahamiana na READY, SET, GO!:
- Hali ya READY –
- Endelea kufuatilia vyanzo rasmi ili upate masasisho ya maagizo ya dharura na uyafuate kwa uangalifu ili uwe salama.
- Endelea kufahamishwa kwa kufuatilia habari za eneo lako na vyanzo rasmi vya taarifa za hali ya hewa.
- Andaa vifaa vya dharura vyenye vitu muhimu kama vile maji, chakula kisichoharibika, vifaa vya huduma ya kwanza, na nyaraka muhimu.
- Tengeneza nafasi ya ulinzi kuzunguka nyumba yako kwa kuondoa vitu vyovyote vinavyoweza kuwaka ndani ya futi 30 kutoka kwa nyumba yako.
- Angalia majirani zako, hasa wale ambao wanaweza kuwa hatarini au wasio na usafiri.
- Ikiwa umeagizwa kuhama, fanya hivyo mara moja na ufuate njia rasmi za uokoaji.
- Hali ya SET – Tishio linaloweza kutokea kwa maisha na/au mali. Wale wanaohitaji muda wa ziada kuhama au walio na wanyama-vipenzi na mifugo wanapaswa kuondoka sasa
- Hali ya GO! – Agizo la uokoaji linalotolewa na huduma za dharura. Agizo la uokoaji linamaanisha kwamba kuna tishio la haraka kwa maisha yako na unahitaji kuondoka sasa hivi! Ni muhimu kufuata maelekezo yote kutoka kwa huduma za dharura ili kuhakikisha kwamba wewe na familia yako mnaondoka kwa usalama.
- Chukua tahadhari zote muhimu na ubaki salama wakati wa tukio hili la moto wa msituni linalokuja. Dhibiti vyanzo vya kuwasha moto:
- Usitupe mabaki ya sigara nje ya dirisha
- Usiburute minyororo nyuma ya malori au trela
- Shughuli yoyote inayoanzisha cheche inaweza kuanzisha moto wa msituni!
Kwa habari zaidi: https://wildfire-austin.hub.arcgis.com/
Vituo vya Kupoeza
Kwa sababu ya joto kali, vituo vya Maktaba na Bustani & Burudani hutumika kama Vituo vya Kupoeza wakati wa saa za kawaida za kazi. Wanyama wa huduma wanaruhusiwa katika vituo vya Jiji. Angalia saa za kazi kabla ya kuwasili.
Ramani ya Vituo vya Kupoeza
Bonyeza hapa ili kuona ramani ya ukubwa kamili ya Vituo vya Kupoeza vya Jiji la Austin.
Maelezo ya Ramani
= Kituo cha Kupoeza cha Bustani kilicho na saa za kazi za kawaida
= Kituo cha Kupoeza cha Maktaba kilicho na saa za kazi za kawaida
= Kituo cha Kupoeza cha Bustani kilicho na saa za kazi zilizoongezwa
= Kituo cha Kupoeza cha Maktaba kilicho na saa za kazi zilizoongezwa
= Eneo limefungwa kwa muda au halipatikani kama Kituo cha Kupoeza
Vituo vya Kaunti:
Vituo vya Jamii vya Kaunti ya Travis vitatumika kama Vituo vya Kupoeza wakati wa saa za kawaida za kazi. Angalia saa na shughuli kabla ya kuwasili.
Maeneo ya Vituo vya Kupoeza vya Kaunti
Kwa maelezo kuhusu kutambua dalili za ugonjwa unaohusiana na joto, na kwa vidokezo vya usalama wa joto, tembelea https://austintexas.gov/heataware
Jaribio la Mifumo ya Kupoeza (Misting Canopies)
Kama mradi wa majaribio, Jiji la Austin linatoa Mifumo ya Kupoeza na maji ya chupa kwa muda katika Republic Square Park. Vituo hivi vinapatikana katika eneo hili pekee kuanzia saa sita mchana hadi saa kumi na mbili jioni (12 - 6 p.m.) wakati kuna Onyo la Joto Kupita Kiasi linalotolewa na Huduma ya Kitaifa ya Hali ya Hewa.
Updated 9:43 a.m. 08/28/2023