Kituo cha Taarifa za Dharura Zinazotumika

Wakati wa janga au dharura, tembelea ukurasa huu ili kupata taarifa rasmi za karibuni zaidi kutoka kwa Jiji la Austin na Kaunti ya Travis kuhusu hatari inayoikabili jamii yetu na hatua za haraka unazopaswa kuchukua ili kukuhifadhi wewe na wapendwa wako salama. Zingatia kualamisha kiunganishi cha ukurasa huu ili uweze kukipata kwa haraka wakati wa janga. Unaweza pia kufuata Austin HSEM katika mitandao ya kijamii:

Twitter - @AustinHSEM

Facebook - @AustinHSEM

Jitayarishe Sasa kwa Ajili ya Dharura

Njia bora zaidi ya kujilinda mwenyewe wakati wa dharura kuu ni kuwa na mpango wa usalama, vifaa, na ufikiaji wa taarifa muhimu muda mrefu kabla haijatokea.

Tembelea ReadyCentralTexas.org ili kujiandikisha kupokea taarifa za dharura, na ujifunze unachoweza kufanya leo ili kujisaidia mwenyewe kuokoka na kupona kwa haraka zaidi kutokana na majanga katika siku zijazo.

 

Ofisi ya Msajili wa Msaada wa Dharura wa Jimbo la Texas

Jisajili kwa Ofisi ya Msajili wa Msaada wa Dharura wa Jimbo la Texas (STEAR). Jisajili kwa STEAR ikiwa wewe, mwanafamilia au rafiki ana hali ya kiafya, mahitaji ya kutembea, au mahitaji ya mawasiliano yanayohitaji msaada wa ziada wakati wa tukio la dharura.

Pakua Programu ya Ready Central Texas

Ofisi ya Jiji la Austin ya Usalama wa Nchi na Usimamizi wa Dharura na Ofisi ya Usimamizi wa Dharura ya Kaunti ya Travis zimeshirikiana kuanzisha programu ya simu ya matayarisho ya dharura.

Programu ya Ready Central Texas huandaa:

  • Ripoti za habari na maonyo
  • Habari za maandalizi
  • Orodha za ukaguzi za mpango wa dharura ili kusaidia kuhakikisha kwamba una kile unachohitaji

Programu hio inapatikana kwenye vifaa vya Android na iOS na ni bure kupakua na kutumia. 

 

Hali

Hakuna arifa zinazotumika. 

 

Updated 2:50 p.m. 04/08/2024